Kusoma Muhtasari
Katibu (Bw. Meshack Nyuha) akisoma Muhtasari kwenye Mkutano wa watumishi wa Mamlaka na Mkurugenzi Mtendaji
Kushiriki Mkutano
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi Mbeya wakati waliposhiriki mkutano baina ya Mkurugunzi mtendaji na watumishi.
Ukaguzi Jengo la Ofisi
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya wakifanya ukaguzi ndani ya jengo jipya kwa ajiri ya ofisi
Mapokezi
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi Mbeya Dkt. Lwitiko Mwakalukwa (kulia) wakati wa mapendekezo ya mabadiriko ya bei za maji.
Ushirikishwaji wa Wanachi Mbeya
Baadhi ya wanachi wa jiji la Mbeya wakisikiliza kwa makini hotuba na maelezo ya viongozi wa EWURA wakati wa zoezi la mapendekezo ya kurekebisha bei za maji
Jengo jipya la Ofisi
Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo la ofisi ya Mamlaka ya Majisafi Mbeya
Chanzo cha Maji Ivumwe
Moja ya chanzo cha maji cha Mamlaka ya Majisafi Mbeya kilichopo Ivumwe. Ni moja ya vyanzo vya chemchemi
Maelezo kuhusu Majitaka Eneo la Kalobe
Mwakilishi wa Shirika la GIZ kutoka Ujerumani akipokea maelekezo ya namna ya umwagaji na utibuji wa Majitaka katika mabwawa ya Mamlaka eneo la Kalobe. Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji na Kulia ni Meneja Biashara wa Mamlaka.

KARIBU MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MBEYA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya (Mbeya WSSA) ipo katika Jiji la Mbeya ikiwa na jukumu kuu la kutoa huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka katika Jiji la Mbeya. Mamlaka ilianzishwa mwaka 1998 kwa Sheria Na. 8 ya mwaka 1997 “Water Works Act Cap 272”, iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.12 ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya ipo katika daraja A. Hii ikimaanisha kuwa ina wajibu wa kugharamia shughuli zote za uendeshaji na matengenezo, kulipa mishahara ya watumishi wake na pia kuchangia kwenye miradi ya uboreshaji na upanuzi wa mitandao ya Majisafi na Usafi wa Mazingira.

DIRA (VISION)

Kuwa Mamlaka Bora katika kutoa huduma endelevu za Majisafi na Usafi wa Mazingira Nchini Tanzania.

DHIMA (MISSION)

Kutoa huduma bora na endelevu za majisafi na usafi wa mazingira zinazokidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa kwa bei nafuu.

KAULIMBIU (SLOGAN)

“Maji kwa Uhai”

MISINGI YA UTENDAJI (CORE VALUES)

a) Wateja Kwanza
b) Watumishi ni Rasilimali namba moja ya Mamlaka
c) Kuwajibika kwa jamii inayotuzunguka
d) Nidhamu katika matumizi ya Fedha
e) Watumishi kufanyakazi kwa pamoja na kujituma
f) Wafanyakazi kuhimizwa kujifunza na kubadilishana maarifa.

Matukio kwa Picha

TOA TAARIFA KUHUSU MIVUJO YA MAJI MAHALI POPOTE

Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira jiji la Mbeya, inawaomba wananchi kutoa taarifa ya mivujo ya maji mahali popote pindi inapotekea. Maji mengi hupotea na kusababisha upungufu wa maji endapo mivujo haitafanyiwa kazi kwa wakati. Taarifa inaweza kutolewa kwa kupiga simu ya bure namba: 0800780050. Pia unaweza kutoa taarifa moja kwa moja kwenye mtandao kwa kubonyeza hapa. TOA TAARIFA YA MIVUJO SASA HIVI

payment

Mkurugenzi Mtendaji

mkurugenzi

Inj. Simeon Shauri

Habari za Karibuni

Kuripoti wizi wa Maji

Mamlaka inatoa kiasi cha Sh. 100,000/= kwa atakae saidia kuonyesha mtu au mteja ambae amefanya maunganisho ya maji yasiyo halali (illegal connection). Kutoa taarifa tafadhali piga bure (0800780050) au Tuma taarifa moja kwa moja kwa kubonyeza hapa. TUMA TAARIFA

KUTUMA USOMAJI WA DIRA

Mteja anaweza kutuma usomaji wake ofisini kwa kutumia mfumo wetu wa kompyuta. Ili kuweza kutuma usomaji tafadhali bonyeza hapa. TUMA USOMAJI WA DIRA