Kufahamu Ankara yako

KWA NJIA YA UJUMBE WA SIMU (SMS)

Kila mwanzoni mwa mwezi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya hutoa Ankara (Bili) za maji kwa wateja na kuzituma kwa njia ya meseji fupi (SMS).

KWA NJIA YA MTANDAO

Ikiwa mteja hajatumiwa Ankara kwa mwezi husika, anaombwa kufika ofisini ili kuangalia taarifa zake na kulipia Ankara husika. Aidha wateja wanaweza kufahamu Ankara zao kwa kubonyeza ukurusa ufuatao.

ANGALIA ANKARA YAKO HAPA

KWA NJIA YA GOOGLE PLAY STORE

Pakua programu ya GePG Tanzania katika Play Store kisha iweke (install) kwenye simu yako. Fungua iyo programu halafu bonyeza linki ya ‘Water’ kisha chagua MBEYA WSSA, utaweka akaunti namba yako ili kuweza kupata ankara za maji.

KUPITIA USSD CODE

Kwenye simu yako bonyeza *152*00#

  1. Chagua no. 1 (Malipo ya Serikali)
  2. Kisha no. 5 (Bili za Maji)
  3. Kisha no. 2 (L-M)
  4. Kisha no. 2 (MBEYA WSSA)
  5. Weka akaunti no yako ili kupata ankara yako