Majibu ya Maswali Mbalimbali

Nawezaje kujiunga na huduma ya maji
Ili upate kuunganishwa na huduma ya majisafi/majitaka inakupasa kufika katika ofisi za Mamlaka ya maji na kujaza fomu. Kisha mafundi wa Mamlaka watafika katika eneo la mteja na kuangalia vifaa (mfano mabomba na vifaa vingine) vitakavyotumika ili kumfikishia maji mteja. Kisha mteja atakiwa kulipia gharama ofisini ili aunganishwe na huduma.

Nawezaje kulipia Ankara yangu
Mteja anaweza kulipia ankara ya maji kwa mawakala wote wa NMB/CRDB/NBC/POSTA au kwa kupitia huduma za simu MPESA/TIGOPESA/AIRTEL MONEY/HALLOPESA. Kulipia kwa mitandao ya simu fuata hatua hizi:-
1. Bonyeza: *150*00# ili kuingia kwenye menyu ya malipo
2. Bonyeza namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
3. Bonyeza namba 5 (Malipo ya Serikali)
4. Bonyeza namba 1 (Ingiza namba ya malipo – Control No)
5. Kisha weka namba ya malipo uliyotumiwa pamoja na bili ya maji
6. Weka kiasi
7. Ingiza namba yako ya siri
8. Thibitisha malipo ya maji.

Mbona sipati bili yangu ya kila mwezi kwa njia ya meseji

Ikitokea mteja hapati bili kwa njia ya meseji itakua ni tatizo la mtandao (network) hivyo mteja naombwa kuangalia bili yake kwa kuingia kwenye tovuti ya mamlaka kubonyeza kwenye menyu ya ankara na kufuata maelekezo. Au anaweza piga simu ya bure (0800780050) na kuuliza ankara yake.

Dira yangu haijasomwa na wasomaji wa dira
Dira inashindwa kusomwa na wasomaji kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwamba dira inakua imefungiwa ndani ya uzio wa nyumba ya mteja. Kama msomaji dira wa Mamlaka hajafika kusoma kuanzia tarehe 01 hadi 15 ya kila mwezi, tafadhali ripoti suala hili mara moja katika ofisi za Mamlaka kwa kupiga simu ya bure (0800780050) ili kuepuka bili kua kubwa wakati itakaposomwa mwezi unaofuatia.

Nimeletewa bili kubwa kulinganisha na miezi ya nyuma / Dira yangu inasoma vibaya

Bili inaeza kua kubwa katika mwezi Fulani kuliko miezi mingine kwa sababu zifuatazo:-

  • Bomba linalodondosha maji kwa matone matone mfululizo
  • Maji yanayovuja katika mtandao wa mabomba ya ndani (Internal Plumbing System).
  • Maji yanayotiririka mfululizo kutokana na kuharibika kwa boya la choo cha kuvuta.
  • Kufua kwenye bomba na maji yakiwa yanaendelea kutiririka.
  • Kupiga mswaki huku bomba la maji likiwa linaendelea kutoa maji.
    Watoto wafundishwe matumizi mazuri ya maji.
  • Kutumia majisafi na salama kwa ajili ya kumwagilia bustani, maji ya umwagiliaji si rahisi kuyakadiria; inashauriwa kutumia kutumia ndoo kumwagilia (Watering can)
  • Kuosha vyombo wakati maji yanaendelea kutiririka. Ni vyema kuchota maji na kuoshea pembeni.

Nawezaje kutoa taarifa ya mivujo ya maji
Ikiwa umeona mvujoa wa maji tunaomba utoe taarifa kwa kupiga simu ya Mamlaka bure (0800780050) au kwa kujaza fomu ya maelekezo inayopatika kwa kubonyeza hapa http://mbeyauwsa.or.tz/index.php/contact-us/

Inachukua muda gani kurudishiwa huduma ya maji toka nilipokatiwa
Ikiwa mteja atasitishiwa huduma ya maji kwa sababu yoyote ile, huduma itarudishwa ndani ya siku 1 – 2 za kazi mara baada ya kulipia gharama za kurejesha huduma.