Malalamiko ya Ankara

Endapo mteja ataona kuna tatizo katika bili aliyopewa (aliyosomewa) na msoma dira au aliyopewa kupitia ujumbe mfupi (SMS), anakaribishwa kufika ofisini ili kuelezea tatizo lake na kuweza kufahamishwa au ikiwa mteja hajatumiwa Ankara kwa mwezi husika, anaombwa kufika ofisini ili kuangalia taarifa zake na kulipia Ankara husika. Aidha wateja wanaweza kuwasiliana na sisi ili kutoa malalamiko kwa njia mbalimbali kama kupiga simu au kujaza fomu maalumu zinayopatikana katika kurusa zifuatazo (Bonyeza hapo chini).