Maunganisho Mapya

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Mbeya ina utaratibu maalumu wa kufuatwa kwa wateja ambao watahitaji huduma ya kuunganishiwa majisafi na majitaka. Utaratibu huo ni kama ifuatavyo.

  • Mteja anaehitaji huduma ya maunganisho ya maji atahitajika kufika ofisini za Mamlaka kitengo cha Maunganisho Mapya (New water connection) na kujaza fomu ya maombi. Au anaweza kupakua fomu hiyo kutoka katika tovuti ya Mamlaka (www.mbeyauwsa.go.tz)

  • Baada ya kujaza fomu watumishi wa Mamlaka watamtaarifu mteja siku ya kufanya ziara kwenye eneo lake na kupima vifaa na miundo mbinu itakayo tumika mpaka kufikishiwa huduma.

  • Mteja ataambiwa gharama za kuunganishiwa maji na vifaa ambazo atatakiwa kuzilipa katika ofisi za Mamlaka.
  • Mtejia ataunganishiwa Maji na kuanza kutumia huduma

ANGALIZO
Gharama zote za maunganisho ya maji zitalipwa katika ofisi za Mamlaka. Kwa msaada zaidi tunaomba upige simu ya bure Namba: +255 784 800076essay writers