Namna ya Kulipa Ankara

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya, inapenda kuwafahamisha watumiaji wa huduma za maji kua kwa sasa malipo yote ya ankara za maji yafanyike kwa njia zifuatazo:-

 • Kupitia Mawakala wa Benki ya NMB

Kwa mawakala wote wa Benki ya NMB walio sehemu mbalimbali za jiji la Mbeya. Mteja atatakiwa kufika kwa wakala wa NMB aliye karibu naye na kumpatia Namba ya Malipo (Control number) na kiwango cha pesa ambacho anataka kulipia huduma ya maji. Wakala atathibitisha taarifa zake kwenye mfumo na kumpatia risiti kwa malipo aliyofanya. Namba hii ya malipo hubadirika kila mwezi bili inapotoka.

 • Kupitia huduma ya MPESA

Kupitia njia ya simu ya mkononi kwa mtandao wa Vodacom (MPESA). Mteja atafuata hatua zifuatazo kuweza kulipia bili kwa njia hii.

 1. Bonyeza: *150*00# ili kuingia kwenye menyu ya MPESA
 2. Bonyeza namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
 3. Bonyeza namba 5 (Malipo ya Serikali)
 4. Bonyeza namba 1 (Namba ya malipo)
 5. Ingiza namba yako ya Malipo (mfano: 994550145524)
 6. Ingiza kiasi (mfano: 20500)
 7. Ingiza namba yako ya siri
 8. Thibitisha malipo
 • Kupitia huduma ya TIGOPESA/HALLO PESA/AIRTEL MONEY

Kupitia njia ya simu ya mkononi kwa mtandao wa Vodacom (MPESA). Mteja atafuata hatua zifuatazo kuweza kulipia bili kwa njia hii.

 1. Bonyeza: *150*00# ili kuingia kwenye menyu ya MPESA
 2. Bonyeza namba 4 (Lipia Bili)
 3. Bonyeza namba 5 (Malipo ya Serikali)
 4. Ingiza namba yako ya Malipo (mfano: 994550145524)
 5. Ingiza kiasi (mfano: 20500)
 6. Ingiza namba yako ya siri
 7. Thibitisha malipo