Usomaji wa Dira

Usomaji wa dira hufanyika kuanzia tarehe 01 hadi tarehe 15 ya kila mwezi. Zoezi hili hufanyika kwa watumishi wa Mamlaka kupita kwa wateja ili kuchukua taarifa mpya za dira. Uniti ambazo mteja wa huduma ya maji ambazo atakua ametumia hukokotelewa kwa kuchukua tofauti ya usomaji mpya kutoa usomaji wa zamani.

Wakati wa zoezi zoezi la kusoma dira watumishi wa Mamlaka huchukua taarifa zingine za dira kama dira kusoma tofauti au kama kuna uharibu wowote wa dira n.k.
Tunaomba wateja kuzingatia yafuatayo:-

    • Kutoa ushirikiano kwa wasomaji dira
    • Kwa wateja ambao dira zao zipo ndaji ya uzio, mtu awepo kwa kipindi hicho cha usomaji wa dira
    • Kuripoti tatizo lolote linalohusu dira kwa msomaji dira

KUTUMA USOMAJI
Mteja anaweza kutuma usomaji wake ofisini kwa kutumia mfumo wetu wa kompyuta. Ili kuweza kutuma usomaji tafadhali bonyeza hapa. TUMA USOMAJI WA DIRA

ZINGATIA
Endapo itatokea msomaji wa dira hakufika katika eneo lako kwa kipindi tajwa hapo juu (tarehe 01 mpaka 15) tafadhali piga namba ya simu bure ya Huduma kwa wateja (0784 800076) ili kuripoti na utapewa maelekezo.